Mmiliki wa Mrina na Wenzake kortini Tuhuma za Uhujumu Uchumi


Mfanyabiashara nchini Tanzania, Maiko Mrina (67) na wenzake wawili wamepandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam na kusomewa kesi ya uhujumu uchumi.

Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka matatu likiwamo la  kuisababishia Serikali ya Tanzania hasara ya Sh30 milioni na kuiba nondo tani nane.

Mbali na Mrina, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni ya uhujumu uchumi namba 140/2019 ni dereva, Ally Athumani (36) mkazi wa Mbagala na mlinzi Shabani Rashidi (57) mkazi wa Mwananyamala wote wa jijini Dar es Salaam.

Katika kesi hiyo, Mrina amesomewa mashitaka yake hospitalini leo Jumanne Desemba 24, 2019 akiwa amelazwa wodi namba mbili katika Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) baada ya kuugua.

Washitakiwa hao walisomewa mashtaka na jopo la mawakili watatu wa upande wa mashtaka, mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Vicky Mwaikambo.

Wakili wa Serikali Mkuu Mkunde  Mshanga akisaidiana na wakili wa Serikali mwandamizi Wankyo Simon na Grory Mwenda, washtakiwa hao wanadaiwa kutenda makosa hayo kati Agosti 29 na 30, 2018 katika eneo la Ubungo.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Sijawahi kusikia mwanasiasa yeyote akipandishwa mahakamani kwa kosa la uhujumu uchumi wakati hata kutoa fedha kwenye hazina bila ruhusa ya bunge pia ni ufujaji na uhujumu uchumi hivyo wapo watu wanafanya makosa ya uhujumu uchumi bila kujua kama wanafanya makosa.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad