Msanii wa vichekesho na mshindi wa mashindano ya Big Brother Afrika 2014, Idris Sultan, amesema sakata la Ofisa wa Kitengo wa kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Tito Magoti, linatia doa kwa jeshi la polisi.
Idris alisema wengi husema
” Naingia kwenye system ili niibadili 10% ndio wanafanikiwa kuwa na msimamo,” aliandika katika ukurasa wake wa Twitter
Aliongezea
” Naelewa ugumu wa kuuvunja mkono unaokulisha ila elewa huo mkono unaweza kukulisha sumu pia,”.
Msanii huyo alisema hivi” Mkuu wa Polisi wewe unajua ustadi mkubwa sana, watoe wasio na busara ofisini kwako. La Tito ni doa,”.
Wengi husema “Naingia kwenye system ili niibadili” 10% ndio wanafanikiwa kuwa na msimamo. Naelewa ugumu wa kuuvunja mkono unaokulisha ila elewa huo mkono unaweza kukulisha sumu pia. Mkuu wa polisi wewe una ustadi mkubwa sana, watoe wasio na busara ofisini kwako. La Tito ni doa.— Idris Sultan (@IdrisSultan) December 23, 2019