Msanii Roma Mkatoliki Aeleza Sababu ya Kushindwa Kurejea Tanzania



Msanii wa muziki Bongo, Roma Mkatoliki amefunguka sababu za kushindwa kurejea Tanzania kwa  wiki nne  tangu aende Marekani huku akikanusha taarifa za kuwa wimbo wake mpya  ndio sababu ya kuogopa kurejea mapema.

Rapa huyo akizungumza na Clouds FM leo amesema sababu kubwa iliyompeleka Marekani ni mualiko maalum alioupata kutoka kwa jamii ya watu wanaozungumza Kiswahili wanaoishi Marekani SUSA mualiko ambao ameeleza kuwa aliupata kama msanii wa Tanzania anayetumia Kiswahili katika kazi zake za kufikisha ujumbe kwa Jamii.

Akizungumzia sababu za kuchelewa kurejea nchini hata baada ya tamasha hilo kumalizika Roma amesema  kwa kuwa yeye ni kijana na anatafuta fursa kila mahali amepata nafasi ya kuangalia fursa zilizopo nchini humo.

 “Marekani kuna fursa nyingi, unapozunguzia tasnia ya burudani huku ndio kama mama, kiukweli  sio sehemu ya kuja Jumatano alafu Alhamisi ukaondoka, kuna fursa nyingi, kuna watu wetu, mashabiki wetu ambao sjawahi kuwaona ni mara yangu ya kwanza kufika huku, kwahiyo utajikuta una vitu vingi vya kufanya” ameeleza Roma.

Ni takribani mwezi sasa msanii huyo amekuwa nchini Marekani na kuonekana katika shughuli mbalimbali nchini humo hali ambayo iliibua maswali ya kwanini hajarejea nchini.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad