Msimamo wa Sumaye Kuhusu Kitabu cha Mkapa


Waziri Mkuu Mstaafu Frederick Sumaye, amempongeza Rais Mstaafu Benjamin Mkapa kwa kuandika Kitabu cha 'My Life, My Purpose' na kueleza kuwa bado anatafuta nakala yake na yeye aweze kukisoma.

Sumaye ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na EATV na EA Radio Digital iliyotaka kufahamu maoni yake kuhusiana Kitabu cha Rais Mkapa ambaye amefanya naye kazi kwa miaka 10, akiwa Waziri Mkuu

Sumaye amesema kuwa " ninampongeza sana kwa kitabu chake hicho bahati mbaya zaidi bado sijakipata ila ninakitafuta ili na mimi nikisome, ila napongeza sana kwa uamuzi wake wa kuandika Kitabu"

"Bahati nzuri asilimia kubwa ya watu waliokisoma wamesema wamechambua kuwa ameandika mambo ya ukweli, nampongeza sana kwa hilo" Amesema Waziri Mkuu Mstaafu Frederick Sumaye
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad