Mwigulu Nchemba Ampa za uso Zitto Kabwe Amtaka Akasome Historia Ajue Ukoloni


Mbunge wa jimbo la Iramba Magharibi (CCM), Mwigulu Nchemba, amempa za uso kiongozi wa chama cha ACT- Wazalendo, zitto Kabwe, kutokana na kauli yake aliyoitoa ya kusherehekea maadhimisho ya Uhuru ni kuhalalisha ukandamizaji.

Nchemba alimjibu Zitto kuwa hakuwepo wakati wa ukoloni na hakupata fursa ya kuhadithiwa na wazazi wake wakati wa ukoloni hali ilivyokuwa.

“Hujasoma historia ujue ukoloni ulikuwaje  kwa kuwa wote kwenye mawazo ya kikoloni unaungana nao. Huwezi kujua thamani ya Uhuru wa taifa lako” aliandika Nchemba kupitia ukurasa wake wa Twitter

Kwa kuwa hukuwepo wakati wa Ukoloni, Hujapata fursa ya kuhadithiwa na wazazi wako wakati wa Ukoloni hali ilikuwaje, Hujasoma hisitoria ujue Ukoloni ulikuwaje kwa kuwa wote wenye MAWAZO ya kikoloni unaungana nao; HUWEZI KUJUA THAMANI YA UHURU WA TAIFA LAKO. pic.twitter.com/tZBuBMZQ87

— Dr.Mwigulu Nchemba (MG) (@mwigulunchemba1) December 8, 2019

Awali, Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amesema  kusherehekea Uhuru na wanaokandamiza Uhuru ni kuhalalisha ukandamizaji.

Zitto ambaye ni Mbunge wa Kigoma Mjini aliandika ujumbe huo kupitia ukurasa wake wa Twitter kuwa kusherehekea Uhuru na wanaokandamiza Uhuru , Uhuru wa mawazo, Uhuru wa kufanya siasa na kuchagua viongozi.

“Rejea uchaguzi wa serikali za mitaa Novemba 2019, Uhuru wa habari (#Azory # Kabendera # Mwanahalisi), Uhuru wa kuishi (#BenSaanane # Lissu  ni kuhalalisha ukandamizaji,” aliandika Zitto.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad