Nilijuwa sita shinda Ballon d’Or hata kabla ya kwenda kwenye sherehe zenyewe” – Van Dijk


Beki bora kabisa duniani kwa sasa, Virgil van Dijk amefunguka kuhusu kukosa tuzo ya mchezaji bora Ballon d’Or huku akisema namna alivyohuzunishwa kwa kuikosa wakati akishuhudia ikienda kwa nyota wa Barcelona, Lionel Messi.

Virgil van Dijk admitted he was disappointed not to win the Ballon d'Or ahead of Lionel Messi

Van Dijk anayekipiga ndani ya klabu ya liverpool alizidiwa kura saba (7) pekee mbele ya mchezaji bora kabisa duniani kwa sasa Messi mwezi katika usiku huo wa tuzo.

Mchezaji huyo mwenye jina kubwa kwa sasa barani Ulaya, aliuambia mtandao wa Mirror kuwa alijua mapema hatokwenda shinda tuzo hiyo ya Ballon d’Or hata kabla ya kufanya maamuzi ya kwenda kwenye sherehe hizo.

Lionel Messi's mum said the Barcelona star did not expect to win the Ballon d'Or last month

“Kiasi fulani nilikuwa nimekata tamaa,” amesema beki huyo aliyesajiliwa kwa dau la pauni milioni 75 kwa kutua Anfield akitokea Southampton miaka miwili iliyopita.

Virgil van Dijk mwenye umri wa miaka 28, ameongeza ”Niliamua, bado lazima niyende kwenye sherehe hizo. Na mwisho wa siku ulikuwa usiku bora sana.”

”Nilizungumza na Messi wakati wa jioni, hayakuwa mazungumzo marefu sana kwa sababu yeye haongei Kiingereza. Lakini yalitosha kwangu kugundua kuwa kuna heshima kati yetu.”

2019 Ballon d’Or points

1. Lionel Messi (Barcelona) – 686
2. Virgil van Dijk (Liverpool) – 679
3. Cristiano Ronaldo (Juventus) – 476
4. Sadio Mane (Liverpool) – 347
5. Mohamed Salah (Liverpool) – 178
6. Kylian Mbappe (Paris Saint-Germain) – 89
7. Alisson (Liverpool) – 67
8. Robert Lewandowski (Bayern Munich) – 44
9. Bernardo Silva (Manchester City) – 41
10. Riyad Mahrez (Manchester City) – 33


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad