ANAOMBA USHAURI : Habari , mimi ni binti wa maika 27, nina mchumba wangu ambaye ameshanitambulisha mpaka kwao na kwetu anajulikana,a nanipenda sana na mimi nampenda. Tatizo lake ni moja tu, kila nikibeba mimba zake ananiambia kuwa nitoe kwani hayuko tayari kuoa kwa sasa tusubiri mpaka ndoa. Yeye ana miaka 32, anafanya kazi nzuri tu na ana kipato kikubwa, amejenga na ana usaifiri wake lakini shida ni hiyo tu.
Nimeshato mimba zake saba mpaka sasa, kaka nimechoka kwani naona kama nitatoa na kizazi, ni mtu wa wanawake sana, namfumania kila siku lakini kila nikimfumania ananiambia kuwa nisijali hao wengine anawachezea mimi ndiyo atanioa. Hivi Kaka nikweli, kama angekua ananipenda kwanini hataki tuzae, kila nikibeba ujauizto ananiambia nitoe, sasa kaka niko njia panda sijui nifanye nini kwani nampenda sana.