Papa Francis: Ni Vizuri Kupunguza Matumizi ya Simu Hasa Wakati wa Chakula


Papa Francis ametoa wito kwa watu kupunguza matumizi ya simu hasa wakati wa chakula.

Ametoa mfano wa Yesu, Maria na Joseph kwamba ni mfano na walikua na mazungumzo mazuri miongoni mwao.

''Inabidi tuanze kuzungumza na familia zetu sio muda mwingi tupo na simu'' anasema Papa Francis.

Papa ni mtumiaji wa mitandao ya kijamii na mara kadhaa huruhusu wafuasi kumpiga picha ama hupiga nao picha.

''Najiuliza mwenyewe ukiwa kwenye familia, unatakiwa kujua jinsi ya kuwasiliani na watoto wanaokula mezani ambapo kila mtu anatumia simu yake, kuna ukimya kama mpo kwenye masi lakini kumbe watu wanatumia simu'' anasema papa.

''Baba, wazazi, watoto, bibi, babu, kaka na dada tunawaomba kufanya zoezi hili la kuongeza mawasiliano lakini sio kwa simu''

Hii sio mara ya kwanza Papa kuzungumza kuhusu matumizi ya simu kukithiri, amewahi pia kuwaambia wafuasi wake kuhusu kutumia simu kwa kupitiliza tena mara nyingi wakati wa mas.

Hii sio mara ya kwanza Papa kuzungumza kuhusu matumizi ya simu kukithiri, amewahi pia kuwaambia wafuasi wake kuhusu kutumia simu kwa kupitiliza tena mara nyingi wakati wa mas

''kuna wakati mchungaji anasema tupandishe imani zetu, sio kupandisha simu zetu na kuanza kupiga picha, ni kitu kibaya sana '' alisema papa mwaka 2017.

''Ni huzuni sana wakati nasherekea masi hapa ndani ya eneo takatifu na naona watu wamepandisha simu zao, hata kwa wachungaji pia , ah tafadhalini''
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad