Polepole Amcheka Sumaye Kuchomoa Betri Asema Alimueleza Kile CHAMA ni Mali ya Mtu Hakusikia


Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Hamphery Polepole amtupia kijembe aliyekuwa Waziri Mkuu Fredireck Sumaye na kumuambia amebaki hana itikadi.

Polepole alimuambi Sumaye kazi ya ushauri hutaipata ukiwa nje ya CCM ” Wanaotushauri na tunazingatia ushauri wao kwa sababu  tunawaheshimu ni wana CCM na kiitikadi tupo pamoja,” aliandika Polepole kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Aliongezea kuwa: ” Sasa umebaki bila itikadi. Ile ni mali ya mtu ni yake, nilikuambia mwache ona sasa unahama mara ya pili,”

Humphrey Polepole
"Mzee nilikwambia, kazi ya ushauri hutaipata ukiwa nje ya CCM wenzako wanaotushauri na tunazingatia ushauri wao kwasababu tunawaheshimu, ni wana CCM na kiitikadi tuko pamoja. Sasa umebaki bila Itikadi. Ile ni mali ya Mtu ni yake, nilikwambia mwache, ona sasa unahama mara ya pili🙆🏽‍♂️"


Leo Novemba 4, 2019 Sumaye ametangaza kukihama chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Pia Sumaye ameweka hadharini siri yake ya kuondoka Chama cha CCM kujiunga na Chadema uamzi alioufanya miaka minne iliyopita.

Akizungumza na waandishi wa habari amesema alijiunga na  Chadema jambo ambalo alikuwa jepesi ikizingatia nafasi aliyokuwa nayo kutokana na kuandamwa na dola yeye binafsi pamoja na familia yake.
Itakumbukwa kuwa Sumaye alihamia upinzani Agosti 2015.
“Nimekuja upinzani kwa lengo la awali la kuimarisha upinzani wa dhati ili  kuchukua dola, Mimi sikuja upinzani kuja  Chadema kutafuta vyeo, wakati nahamia upinzani tayari vyama vilikuwa vimepanga wagombea tayari.”
Pamoja na mambo hayo Sumaya ametangaza uamzi wa kujivua uanachama wa chama hicho huku Mratibu wa Chadema Kanda ya Pwani, Casmiri Mabina ambaye aliambatana na sumaye katika mkutano huo akiwasilisha barua kwa chama chake kuomba kujiondoa katika hiyo kutokana na yaliyojiri.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad