Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto, amesema kuwa kufeli kwa moyo na kukosa msaada wa haraka wa matibabu, ndiyo chanzo cha kifo cha Sheikh Rashid Bura, ambaye ni mmiliki wa shule za Zamzam mkoani humo.
Kamanda Muroto amebainisha hayo leo Disemba 27, 2019, na kusema kuwa mara baada ya kupata taarifa hiyo, Polisi walifika eneo la tukio na kwamba hawakukuta viashiria vyovyote vya mauaji, badala yake uchunguzi umebainika kuwa alifariki baada ya kukosa msaada kwa kuwa hali hiyo ilimkuta ofisini akiwa peke yake.
"Taarifa za kiuchunguzi za awali zinaonesha kifo chake kimetokana na kufeli kwa moyo na kwakuwa alikuwa ofisini kwake hakupata msaada na simu yake ilikuwa imezima ndugu zake walishindwa kumpata na ofisini tulikuta kupo salama na hakukuwa na wizi wowote uliofanyika" amesema Kamanda Muroto.
Kwa mujibu wa Kamanda Muroto, mwili wa Bura uligundulika siku ya Disemba 25, 2019, na kuwataka waandishi wa habari, kuacha kusambaza taarifa ambazo wanakuwa hawajazithibitisha kutoka kwenye vyanzo halisi likiwemo Jeshi la Polisi ama kwa Daktari