Rais Macron Auita Ukoloni Kuwa ni Kosa kubwa
0
December 22, 2019
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameungana na mataifa mengine manane ya Afrika Magharibi kutangaza mabadiliko makubwa ya sarafu moja ya kikanda ikiwa ni pamoja na kuondoa mahusiano ya sarafu hiyo na Ufaransa.
Macron, akiwa mjini Abidjan amesema ukoloni barani Afrika ulikuwa ni kosa kubwa lililofanywa na Ufaransa, huku akitoa mwito wa kuanzishwa mahusiano mapya na Ufaransa.
Haikuwa mara ya kwanza kwa Macron kuelezea majuto hayo kwa niaba ya Ufaransa kuhusiana na enzi za ukoloni.
Wakati wa kampeni za urais, alipamba vichwa vya habari pale alipoufananisha ukoloni wa Ufaransa nchini Algeria kuwa ni uhalifu dhidi ya ubinaadamu.
Ziara ya Macron nchini Ivory Coast inakuja wakati viongozi wa kikanda walipokutana kutangaza kubadilisha jina la sarafu hiyo ya Faranga ya CFA.
Tags