RIPOTI: Umaskini Wapungua Tanzania Kwa Asilimia 2



Matokeo ya tathmini ya umaskini kwa kutumia Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara ya mwaka 2017/18 na tafiti zilizofanywa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) na Benki ya Dunia yameonesha ndani ya miaka 4 umaskini umepungua kwa asilimia 2

Matokeo yameonesha kuwa, umaskini wa mahitaji muhimu umepungua kutoka asilimia 34.4 mwaka 2007,  asilimia 28.2 mwaka 2012, hadi asilimia 26.4 mwaka 2018

Umaskini wa chakula umepungua kutoka asilimia 22 mwaka 1991/92, asilimia 19 mwaka 2000/01, asilimia 17 mwaka 2007, asilimia 10 mwaka 2011/12 hadi asilimia 8.0 mwaka 2017/18

Aidha, katika taarifa hiyo Benki ya Dunia ilieleza kuwa karibu nusu ya idadi ya watu nchini Tanzania kila mmoja anaishi chini ya dola 1.90 kwa siku

Ripoti hiyo imeonesha kiwango cha jumla cha elimu na upatikanaji wa huduma za msingi kimebaki chini, hasa kwa maskini na kwa wale wanaoishi vijijini
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad