Sababu na athari zitokanazo na kitambi



Utafiti  umegundua  kwamba  kuna  idadi  kubwa  sana  ya wanawake  na  wanaume  wanao  sumbuliwa  na  tatizo  la  kuwa  na matumbo  makubwa  kiasi  ama  vitambi  kwa  lugha  nyingine. Uchunguzi wetu  umetuwezesha  kubaini  kuwa  katika  watu  kumi  wanao  tembea bararani  angalau  watatu  kati yao  wanasumbuliwa na  tatizo la kitambi.

Sababu  kuu  za tatizo la  kitambi  ni  pamoja  na;
Ulaji  mbovu  wa  vyakula ( Ulaji usio zingatia  mlo  kamili ).
Ulaji  mbovu  wa  vyakula  unajumuisha   ulaji  wa  vyakula  vya  aina moja  kwa  wingi  kupita  kiasi  bila  kuzingatia  aina  nyinginezo, mfano  ulaji  wa  vyakula  vya  mafuta  mafuta  kwa  wingi kupita kiasi.
Unywaji  wa  pombe  kupita  kiasi
Kutofanya  mazoezi  ya  mwili  na  viungo pamoja  na  sababu  nyinginezo.


Athari  za  tatizo  la  kitambi  ni  pamoja  na :
Kuwa  katika  hatari ya  kushambuliwa  na  magonjwa  ya  hatari kama  vile  kisukari, moyo  na  presha.
Kutokuwa  na  uwezo  wa  kumudu  tendo  la  ndoa (  kwa  wanaume )
Kupunguza   mvuto  wa  kimapenzi (  kwa  wanawake na  hata  wanaume  pia  )
Kupoteza  fedha  na  muda  mwingi  katika  kuhangaika  kutafuta tiba  ya  tatizo   pamoja  na  athari  nyinginezo  lukuki.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad