SAKATA la Mkurugenzi Kampuni ya Ujenzi Kuzirai na Kuanguka Mbele ya Waziri


Dodoma. Mkurugenzi wa kampuni ya Scol Building Contractors Limited ameanguka na kuzirai mbele ya Waziri wa Tamisemi, Selemani Jafo baada ya kubanwa kuhusu ucheleweshaji wa ujenzi wa barabara ya Martin Luther hadi Swaswa mjini Dodoma.

Tukio hilo limetokea leo Jumatano Desemba 4, 2019 baada ya Jafo  kutembelea ujenzi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilomita nane iliyotakiwa kukamilika Agosti lakini ukaongezwa muda hadi Oktoba, 2019. Alizirai baada ya kuelezwa na Jafo kuwa kusuasua kwake  kutasababisha asipewe kazi nyingine za ujenzi wa barabara.

Kutokana na kuchelewa huko mkandarasi huyo  amekatwa Sh80 milioni na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (Tarura).

Licha ya kujitetea kuwa wamejenga katika miradi mingi nchini ikiwemo katika jimbo la Kisarawe ambalo mbunge wake ni waziri huyo wa Tamisemi, waziri huyo alikataa na kubainisha kuwa uwezo wa kampuni hiyo ni mdogo.

Baada ya hoja hiyo kupanguliwa na Jafo, mkurugenzi huyo alijitetea kuwa anakwamishwa na upatikanaji wa malighafi.

“Si watu wengi wanaweza kutumia hii nyenzo, hili jiwe hili linatoka Lugoba, Sisi tunataka tufanye kazi nzuri,” alijitetea mkurugenzi huyo.

Mwananchi
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad