Serikali Imepeleka Kusudio la Kukata Rufaa kwa Hukumu iliyomwachia Abdul Nondo, Wanataka Afungwe


Serikali imeweka kusudio la kukata rufaa ya kesi ya Jamhuri, dhidi ya aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Mtandao wa wanafunzi wa vyuo vikuu, Abdul Nondo, ambapo kwa sasa kesi hiyo itapelekwa Mahakama ya Rufaa ya Tanzania.


Nondo ambaye alikuwa anakabiliwa na mashtaka mawili, likiwemo la kuchapisha taarifa za uongo mitandaoni, pamoja na kutoa taarifa za uongo, Disemba 23 mwaka huu, Mahakama Kuu kanda ya Iringa, ilimuachia huru katika kesi ya rufaa iliyokatwa na Jamhuri baada ya kuonekana, hoja za rufaa za upande wa Serikali, kutokuwa na mashiko.

Ikumbukwe kuwa Novemba 5 mwaka 2018, Mahakama ya Hakimu Mkazi Iringa, ilimemuachia huru Nondo kutokana na Jamhuri kushindwa kuthibitisha mashtaka mawili yaliyokuwa yanamkabili


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad