No title



Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), limetakiwa kuongeza bidii kwenye kazi, kuepuka vitendo ya rushwa na hujuma na kuboresha huduma zao ili kuwavutia watu wengi kusafiri na ndege zao.

Kauli hiyo imetolewa na Rais John Magufuli leo Jumamosi Desemba 14, alipokuwa akizungumza katika hafla ya kuipokea ndege ya shirika hilo aina ya Bombardier Dash8 – 400 katika Uwanja wa Kimataifa wa Mwanza baada ya kuachiwa nchini Canada iliposhikiliwa baada ya kutengenezwa.

“Nitoe wito kwa kwa uongozi na utumishi wa ATCL kuongeza bidii kwenye kufanya kazi msibweteke kwa mafanikio mliyoyapata endelee kuchapa kazi epukeni vitendo vya rushwa na hujuma lakini muhimu zaidi boresheni huduma zenu ili kuwavutia wengi kusafiri na ndege zenu hasa katika kipindi hiki ambacho mmeanza kufanya safari za kimataifa kwani msipofanya hivyo itakuwa vigumu kwenu kushindana na mashirika mengine.

“Ninalipongeza sana shirika letu la ndege hata ninyi mtapigwa vita sana mnaweza mkaambiwa ni wabaya yani mabinti wazuri hivi unaweza ukasema ni wabaya jamani mnapendeza sana Air Tanzania tembeeni kifua mbele na nguo zenu ni nzuri, shepu zenu ni nzuri, lugha zenu ni nzuri na mioyo yenu ni mizuri,” amesema Rais Magufuli.

Aidha ameongeza kuwa katika siku za usoni serikali ina mpango wa kununua ndege ya mizigo ili Watanzania waweze kufanya biashara kwa haraka zaidi.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad