Beno Kakolanya, mlinda mlango namba mbili wa Simba ameonyesha ukomavu kwenye mechi yake ya kwanza akiwa na Simba kwa kuvunja rekodi ya mlinda mlango namba moja Aish Manula ndani ya dakika 90 za kwanza kukaa langoni bila kufungwa.
Kwenye mchezo wa kwanza wa ligi kwa Manula kukaa langoni dhidi ya JKT Tanzania alishindwa kutoka na ‘Clean Sheet’ licha ya ushindi wa mabao 3-1 ila Kakolanya ameanza kwa kutoruhusu bao huku timu hiyo ikishinda jumla ya mabao 4-0 dhidi ya Lipuli na mechi zote zilichezwa uwanja wa Uhuru.
Kakolanya amekaa benchi kwenye mechi 10 mbazo ni sawa na dakika 900 ambazo zote Manula alikaa langoni na kufungwa jumla ya mabao matatu amepotezwa na Kakolanya kwenye dakika 90 za mwanzo.
Kocha wa makipa ndani ya Simba, Mwarami Mohamed amesema kuwa makipa wote ni bora utofauti wao ni namba tu ndani ya kikosi.
“Makipa wote wa Simba ni bora na watapata nafasi, tofauti ni kwamba Manula ni kipa namba moja wa Simba kwa mengine wapo sawa na kila mmoja ana kitu chake cha pekee,” amesema Mohamed.