Tabia za Watu Wenye Usaliti Katika Mahusiano ya Kimapenzi



Usaliti ni jambo baya sana katika mahusiano, usaliti si ujanja japo wengi wanaowaza kusaliti huwa wanajiona wajanja. Wanajiona wamefanikiwa pale ambapo wanasaliti na wenza wao kutogundua kama wanasalitiwa.

Siku zote anaesaliti huwa anajiona mjanja kwamba yeye anasaliti wakati mwenzake hasaliti. Kwa asilimia kubwa wanaume hujiona kama usaliti ni halali yao, wanataka wao wasaliti lakini wapenzi wao wasithubutu kusaliti.

kwanini hawataki wenzi wao wasaliti? Eti wanaumia, hakuna kitu kinacho mchukiza mwanaume kama kusalitiwa. Kusaliti asaliti yeye, akisaliti mwenzake ni kosa la jinai anaona amedhalilishwa.

Anajisikia fedheha kwamba mpenzi wake amemuonaje? Amemchukuliaje? Hajakamilika idara gani? Anawaza sana na kujiuliza jamii nzima inayojua kitendo hichoitamtazamaje?

Hapo ndio unakuta mwanaume anaamua kuchukua uamuzi mgumu ikiwemo hata kuhatarisha maisha ya mwenza wake.

Zifuatazo ni dalili za usaliti:

Kutopenda kuchimbwa.
Mara nyingi anaesaliti huwa hapendi kuchimbwa mambo kwa undani, anahofu anaweza kuchanganya madawa, hupenda mazungumzo mafupi na moja kwa moja.

Hapendi kuulizwa maswali mengi, ukimuuliza anayakwepa haraka na kutaka kukupeleka kwenye mazungumzo anayo yataka yeye.

Ukimuuliza kuhusu mipango yenu, ukimuuliza kuhusu mustakbali wa penzi lenu baadae hukuondoa kwenye mstari na kukufanya usiwe na hamu ya kumuuliza.

Hapendi ujue ratiba zake.
Mara nyingi mtu ambae ana lake jambo huwa hapendi ujue ratiba yake, anataka usimzoee, iwe anafanya maamuzi yake kulingana na yeye mwenyewe anavyojua, ikitokea unaijua ratiba yake atakuwa ni mtu wa kutoa udhuru kila wakati.

Leo atakuambia kuna mgonjwa anakwenda kumuona, kesho atakwambia kuna vikao na wafanyakazi wenzake, siku nyingine atakuambia gari imepata pancha analazimika kusubiri mafundi hadi wafike ndio aweze kuanza safari.

Simu yake ni kituo cha polisi.
Anaesaliti mara nyingi hapendi kuacha simu yake kiholela, simu inakaa mfukoni kwake hata kama hakuna ulazima wa kufanya hivyo, mpo nyumbani mpo kwenye mazungumzo ya kifamilia yeye yake ipo mfukoni.

Imetolewa mlio hataki uione inaita maana inawezekana akatumiwa ujumbe, picha na mambo mengine ya kimapenzi.

Anaejiamini na yupo na yupo kwenye uhusiano imara hana sababu ya kuficha ficha simu yake anaiweka hadharani.

Mwingine atakusetia simu yake ukimpigia kila wakati inaonekana inatumika, kumbe yeye ndio anatumika wakati huo anakusaliti.

Anachat sana.
Wanaosaliti wengi wao hupenda kutumia meseji katika mawasiliano yao, yaani amewazoesha michepuko yake wote kusaliti hapendi kupokea sana simu, zaidi anapenda kuchati hivyo ni rahisi kuwasiliana na michepuko.

Mwisho hakutambulishi kwa watu wake wa karibu.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad