TANZIA: Mhubiri na Mwinjilisti Reinhard Bonnke Afariki Dunia


Bonnke ambaye ni raia wa Ujerumani amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 79 akiwa amezungukwa na familia yake

Atakumbukwa kwa kuweka rekodi ya wahudhuriaji wengi katika mikutano yake ambayo aliyoifanya kwenye mataifa mbalimbali ya Afrika ikiwemo Tanzania

Inaelezwa kuwa kwa wakati wote aliofanya kazi hiyo aliwafanya watu milioni 79 kuwa Waumini wa dini ya Kikristo

Mwaka 2001 alifanya mkutano mkubwa katika viwanda vya Jangwani Jijini Dar huku mkutano wake wa Lagos, Nigeria(2000) ukiweka rekodi ya wahudhuriaji milioni 1.6
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad