UNAAMBIWA Wanaume Wenye Michepuko Hatarini Kupata Tezi Dume




Msimamizi wa upimaji wa tezi dume na virusi vya Ukimwi, wilayani Pangani, Dkt. Paul Chabai amebainisha kuwa moja ya sababu ya wanaume kupata ugonjwa wa tezi dume ni kuwa na msururu wa wanawake wengi ‘Michepuko’

Akizungumza na Nipashe jana, amesmea kuwa wanaume wenye wapenzi wengi wanajiweka katika hatari zaidi ya kupata tezi dume hasa wakijamiiana bila kutumia kinga.

” Unajua tezi dume ni uvimbe ambao huwa unajitokeza pembeni karibu na sehemu za siri na haujitokezi haraka. unachukua muda mrefu na mwanaume anapokutana na wanawake wengi ndivyo anavyojiwekea hatari ya kupata ugonjwa huu” amesmea Dkt. Chabai.

 Na ameongeza kuwa tezi dume haiambukizi kwa mbu kama ngiri maji (mabusha) bali ni uvimbe ambao hujitokeza na huchukua muda mrefu.

” Naomba wanaume tujiwekee utaratibu wa kwenda hospitalini kupima afya zetu kwani ukigundulika mapema ni rahisi kupata tiba lakini ukichelewa tatizo linazidi kuwa kubwa” ametilia mkazo Dkt. Chabai.

Amesema tezi dume ikiwa katika hatua za mwanzo, mgonjwa anaweza kupatiwa tiba ya vidonge na madaktari bingwa kwa kufuatilia utaratibu wa vipimo vya ugunduzi lakini kama ikifika hatua za juu zaidi, mgonjwa hufanyiwa operesheni ya kuondoa kabisa tezi dume.

Amebainisha changamoto iliyopo juu ya kukabiliana na ugonjwa huo ni elimu ndogo kwa wanaume juu ya tezi dume, hali inayosababisha kuwepo kwa idadi ndogo ya wanaume wanaojitokeza kupima na wengi wao ugonjwa unakuwa tayari umekomaa.

Adha amesema sababu nyingine inayosababisha ugonjwa huu ni uwepo wa saratani japo huwa inahitaji kupata vipimo vikubwa.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad