Mwafrika Atwaa Taji La Miss Universe 2019, Mtanzania Chali


Usiku wa kumkia leo Tarehe 9, Desemba 2019 Mrembo Zozibini Tunzi kutoka Afrika ya kusini amefanikiwa kunyakuwa taji la Miss Universe mwaka 2019

Shindano hili kilofanyika Nchini Ufilipino katika jiji La Madila likishirikisha jumla ya warembo 90 kutoka sehemu mbalimbali ulimwenguni

Zozibini alifanikiwa kuingia tatu bora na kuwashinda wenzake wawili kutoka Puerto Rico Madison Anderson (Amekuwa mshindi wa pili) na Sofía Aragón kutoka Mexico ambaye amekuwa mshindi wa tatu

Zozibini amechukua mikoba ya taji hilo kutoka kwa raia wa Ufilipino, Catriona Gray ambaye alilitwaa mwaka 2018.

Zozibini anakuwa raia wa tatu wa Afrika Kusini kutwaa taji hilo baada ya Margaret Gardiner mwaka 1978, and Demi-Leigh Nel-Peters mwaka 2017.


Tanzania iliwakirishwa na mrembo Shubila Stanton ambaye hakufanikiwa kufika kwenye kumi bora ya mashindano hayo
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad