Vitisho Dhidi ya Sekta ya Habari vyazidi


Matukio ya vitisho dhidi vyombo vya habari yameongezeka kutoka manane mwaka 2015 hadi kufikia 28 mwaka 2019, kwa mujibu wa ripoti ya Baraza la Habari Tanzania (MCT).

Ripoti hiyo ya Uchunguzi wa Kuingiliwa kwa Uhuru wa Habari iliyotolewa jana inaonyesha kuwa matukio yaliyosajiliwa ya ukiukwaji wa uhuru wa habari yameongezeka.

Ripoti hiyo ililenga kuchunguza madai kutoka kwa wanachama wake na wadau kuhusu ukiukwaji wa uhuru wa habari unaofanywa na watu wasiojulikana, mamlaka za Serikali, vyombo vya dola na watu wanaojiita wanaharakati na vyombo visivyo vya kiserikali.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, nchi ilikuwa na matukio manane mwaka 2015, wakati mwaka 2016 yalifikia matukio 32 huku 2017 yakifikia 23 na mwaka 2018 yakifikia 18.

“Idadi ya ukiukwaji ni kubwa kuliko matukio yaliyoripotiwa kwa sababu matukio ambayo hayajathibitishwa hayajaingizwa katika ripoti ya ukiukwaji wa uhuru wa habari (PFVR),” alisema ofisa wa MCT katika mahojiano.

Nyaraka na mahojiano yameonyesha kwamba Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016, Sheria ya Makosa ya Mtandao ya 2015 na Kanuni za Maudhui ya Mtandao za mwaka 2018 ni miongoni mwa sheria na kanuni zinazobariki ukiukwaji huo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad