Vyama vya Siasa Vyataka Uhuru wa Demokrasia


Na. Amiri kilagalila-Njombe

Baadhi ya wanasiasa mkoani Njombe wamesema Tanzania inapaswa kujisahihisha katika maeneo ya utawala bora,rushwa na kilimo katika kusherekea miaka 58 ya uhuru wa tanganyika.

Mwaka 1961 Disemba 9 Tanganyika ilipata uhuru wake ku toka kwa muingereza na kuanza kujitawala katika mambo yake lakini wanasiasa mkoani Njombe wametoa maoni yao katika nyanja za kisiasa na maendeleo ambapo katibu wa siasa na uenezi ccm mkoa wa Njombe Erasto Ngole akipongeza maendeleo yaliyopatikana kwa miaka 58 ya uhuru huku suala la rushwa likitakiwa kuendelea kupigwa vita.

“Mahali pa kujisahihisha kwa sasa ni eneo la rushwa,tumeona mheshimiwa anavyopigana katika swala hili la rushwa lakini bado watanzania hatujapona ugonjwa wa rushwa,lakini kisiasa Tanzania inakwenda vizuri kwasababu matokeo ya siasa inatakiwa yaakisi maendeleo ya nchi lakini vipo vitu vidogo vidogo ambavyo havijakaa vizuri hasa kwa wenzetu wa upinzani”Alisema Erasto Ngole

Lukule Mponji ni Mwenyekiti wa chama chaTLP mkoa wa Njombe anasema demokrasia ya vyama vingi nchini inaendelea kuminywa hatua ambayo tanzania inatakiwa kujisahihisha.

“Wakulima tumeanza kupuuzwa sasa hivi kilimo kinakufa,hawa watoto wanaoingia darasa la kwanza wana miaka mitano wanapotoka chuo kikuu hawawezi kilimo tuwe na somo la kilimo”alisema Mponji

Mwenyekiti mpya wa CHADEMA  mkoa wa Njombe Rose Mayemba pamoja na kukiri hatua kubwa iliyopigwa kimaendeleo nchini lakini bado anasema suala la utawala bora limepewa kisogo jambo ambalo linakandamiza demokrasia nchini.

“Leo tunaona watu hawako huru,leo tunapozungumzia uhuru tunazungumzia kuminywa kwa vyama vya siasa,tangu tumeanza mwaka 2015 mpaka leo vyama vya siasa vimezuiliwa kufanya mikutano, vyama vimezuiliwa kujenga vyama vyao,lakini leo tunazungumzia uhuru ambao lengo lake kubwa ilikuwa ni kuhakikisha tunajenga misingi ya haki,amani,mshikamano leo hakuna amanikwa hiyo hakuna kitu kitakaa sawa kama hakuna misingi ya utawala bora na uwajibikaji”alisema Rose Mayemba

Lakini baadhi ya wananchi mjini Njombe wanasema kwa sasa nchi ya Tanzania imeweza kupiga hatua za kimaendeleo kwa kuweza kujenga miundombinu ikiwemo ya bara bara na afya.

Sherehe za miaka 58 ya uhuru wa Tanganyika kitaifa zimefanyika jijini mwanza kwa kuhudhuriwa na rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli pamoja na viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa na serikali.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad