Wahukumiwa Jela kwa 'Kuzamia' Nchini Afrika Kusini



Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewahukumu mwezi mmoja jela na kulipa faini ya Tsh. 50,000  Raia wa Tanzania 52 waliozamia kwenda Afrika Kusini kinyume na Sheria.

Hukumu hiyo imesomwa na Hakimu Mkazi, Victoria Mwaikambo baada ya washitakiwa hao kusomewa mashitaka yao na Mawakili wa Idara ya Uhamiaji Tanzania, Shija Sitta na Godfrey Ngwijo.

Mara baada ya kukiri makosa hayo, Hakimu Mwaikambo amewapata na hatia kwa makosa ya kutoka Nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kinyume cha Kanuni ya Uhamiaji ya 20(3)(a) pamoja na Kanuni ya 37 ya Kanuni za Uhamiaji G.N 657 ya mwaka 1997.

Washitakiwa hao 52 wanadaiwa kwa nyakati tofauti waliingia isivyo halali Afrika Kusini bila kufuata taratibu za Idara ya Uhamiaji Tanzania

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad