Wakala wa Barabara za vijijini na mjini TARURA wilayani Igunga Mkoani Tabora wanatarajia kutumia kiasi cha shilingi Milioni 455 kutengeneza Barabara 2 za kiwango cha lami mjini Igunga yenye urefu wa km 1.3 kwa mwaka wa fedha 2019/2020
Hayo yamesemwa na meneja wa TARURA wilayani humo Mhandisi Sadick Karume katika kikao cha baraza la madiwani wa halmshauri ya wilaya huyo
Karume ametaja Barabara zitakazotengenezwa ni Igunga-mbutu yenye urefu wa km1.0 itakayogharimu kiasi cha shilingi Milioni 380 na ile ya CCM -SingidaRoad yenye urefu wa km 0.3(mita 300)ambapo itagharimu kiasi cha pesa shilingi Milioni sabini na tano
Pia amesema ujenzi wa Barabara hizo ni sehemu ya mkakati a wakala huyo kuboresha Barabara zote za mji huo ikiwemo kuzifanyia matengenezo makubwa Barabara mbovu zote zinazounganisha vijiji na kata zote wilayani humo
Aidha amesema matengenezo hayo pia yataambatana na ujenzi wa mifereji makaravati na madaraja ili barabara hizo ziweze kupitika wakati wote Huku akibainisha mchakato wa kuanza ujenzi wa Barabara ya mbutu- isakamaliwa tayari umekamilika
Wakichangia hoja baada ya kuwasilishwa kwa taarifa ya utekelezaji miradi ya TARURA baadhi ya madiwani wamelalamikia barabara za Kata zao ambazo hazipitiki kutoingizwa katika mpango wa matengenezo kwa mwaka ujao wa fedha
Nao baadhi ya madiwani waloochangia hoja ni Elisha Anthony wa Kata ya kining'inila) Jilala Mipawa Kata ya humba na mwenyekiti wa halmashauri hiyo Lucas Bugota wameeleza kuwa barabara nyingi za vijijini zinatengenezwa kwa kiwango cha chin sana kiasi kwamba hazikawii kuharibika hivyo wameishauri TARURA kuobgezewa bajeti ili iweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo na kuwataka wataalamu wa TARURA kutumia utaalamu wao ili barabara zinazojengwa ziweze kudumu tofauti na hali ilivyosasa
Kwa upande wake Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Peter Onesmo ambae pia ni diwani wa Kata ya choma amemtaka meneja wa TARURA wilayani humo kufanyia kazi ushauri anaopewa na madiwani ili kuepusha malalamiko ya mara kwa mara kutoka kwa wananchi.