Wamevuna Mamilioni ya Watazamaji



TUMEBAKIZA siku chache kuumaliza mwaka 2019. Ni muda muafaka wa kila mtu kujifanyia tathmini ili kuona kama malengo yametimia au la! Kama yalitimia ni jambo jema sasa kuweka mipango mingine, lakini kama hayakutimia ni muda muafaka pia kujipanga upya kwa ajili ya mwaka ujao wa 2020.

 

Si vibaya kutazama kile wasanii wetu walichopanda na kile walichovuna kwa mwaka huu. Kwenye makala hii tutaangazia wale waliofanikiwa kuvuna mamilioni ya watazamaji kupitia video zao kwenye Mtandao wa Kijamii wa YouTube.

 

Hapa tutazitazama zile video ambazo zilitoka tangu Januari hadi Desemba, mwaka huu na idadi ya views (watazamaji) zilizopata kuanzia milioni tano na kuendelea;

 

MY BOO REMIX -HARMO X Q CHILLA

Video hii iliyoongozwa na Director Hanscana. Ilipandishwa kwenye Mtandao wa YouTube, Julai 23, mwaka huu na hadi ninaandika makala hii, juzi ilikuwa na watazamaji zaidi ya milioni 5.5.

 

NITEKE – HARMO

Ngoma hii inapatikana kwenye EP ya Harmo aliyoachia mwaka huu ya Afro-Bongo. Video hii iliyoongozwa na Director Kenny ilipandishwa YouTube, Machi 26, mwaka huu na hadi juzi ilikuwa na watazamaji zaidi ya milioni 5.9.

 

MAAJABU – MBOSSO

Video ya ngoma hii iliongozwa na Director Kenny na kuwekwa YouTube, Juni 14, mwaka huu ambapo hadi juzi ilikuwa na watazamaji zaidi ya milioni 6.1.

 

NEVER GIVE UP – HARMO

Mei 23, mwaka huu ndiyo siku ilipopandishwa YouTube. Video hii imeongozwa na Director Kenny na hadi juzi ilikuwa na watazamaji zaidi ya milioni 7.2.

 

BABA LAO – MONDI

Video ya Baba Lao ilipandishwa YouTube, Novemba 8, mwaka huu, siku chache kabla ya fainali ya Tamasha la Wasafi Festival jijini Dar. Tangu siku hiyo hadi juzi, video hii iliyoongozwa na Director Kenny imefanikiwa kujikusanyia watazamaji zaidi ya milioni 8.2.

 

HALLELUJAH – NANDY X WILLY PAUL

Ukiachilia mbali ngoma yao nyingine ya Njiwa ambayo ilitazamwa na wengi, video yao ya Hallelujah iliyotengenezwa na Director Trued waliiachia kwenye YouTube, Machi 29, mwaka huu na hadi juzi ilikuwa na watazamaji zaidi ya milioni 8.7.

 

ATARUDI – HARMO

Mzigo mwingine wa Harmo ni huu uliowekwa kwenye YouTube, Agosti 19, mwaka huu ukiwa umeongozwa na Director Kenny. Hadi juzi video hii ilikuwa na watazamaji zaidi ya milioni 11.

 

KANYAGA – MONDI

Video hii iliyoongozwa na Director Kenny na kuwekwa YouTube, Juni 25, mwaka huu, hadi juzi ilikuwa na watazamaji zaidi ya milioni 11.2.

 

TAMU – MBOSSO

Video nyingine ya Mbosso iliyotisha ni hii ya Tamu iliyotengenezwa na Director Kenny na kupandishwa YouTube, Januari 18, mwaka huu ambapo hadi wikiendi iliyopita ilikuwa na watazamaji zaidi ya milioni 12.

 

MMMH – RAYVANNY FT WILLY PAUL

Video hii iliyoongozwa na Director Ivan iliwekwa YouTube, Februari 26, mwaka huu na hadi juzi ilikuwa na watazamaji zaidi ya milioni 12.3.

 

KAINAMA – HARMO X BURNA BOY X MONDI

Hapa walikutana mastaa watatu wakubwa Afrika. Video yao hii iliyoongozwa na Director Kenny ilipandishwa YouTube, Machi 10, mwaka huu na hadi wikiendi iliyopita ilikuwa na watazamaji zaidi ya milioni 12.8.

 

THE ONE – MONDI

Video hii iliyotengenezwa na Director Kenny iliwekwa YouTube, Aprili 21 na hadi juzi ilikuwa na watazamaji zaidi ya milioni 17.4.

 

PEPETA – RAYVANNY X NORA FATEHI

Video hii inayomilikiwa na wote iliongozwa na Director Abderrafia na kuwekwa YouTube, Septemba 9, mwaka huu, hadi wikiendi iliyopita ilikuwa na watazamaji zaidi ya milioni 24.

 

TETEMA – RAYVANNY FT MONDI

Video hii ya jamaa hawa ilikuwa video ya taifa. Iliongozwa na Director Kenny na kuwekwa YouTube, Februari 7, mwaka huu. Hadi wikiendi iliyopita ilikuwa na watazamaji zaidi ya milioni 34.7.

 

INAMA – MONDI FT FALLY IPUPA

Ni miongoni mwa video za Mondi zenye mafanikio makubwa. Video hii iliyoongozwa na Director Jessica Francois na Director Kenny iliwekwa YouTube, Juni 9, mwaka huu. Hadi wikiendi iliyopita ilikuwa na watazamaji zaidi ya milioni 41.

 

YOPE REMIX – INNOSS’B FT MONDI

Hii ndiyo video ya mwanamuziki wa Bongo Fleva iliyotazamwa zaidi. Video hii imeongozwa na Director Kenny na kuwekwa YouTube, Septemba 7, mwaka huu. Hadi wikiendi iliyopita ilikuwa imetazamwa na watu zaidi ya milioni 43.

 MAKALA: SIFAEL PAUL



Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad