Wanafunzi wanaofanya vizuri somo la Kiswahili UDSM kuwezeshwa



Chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM) kwa kushirikiana na Kampuni ya Kutengeneza Mabati ya ALAF Afrika zimeendesha shindano la kuwawezesha wanafunzi wanaofanya vyema katika masomo ya Kiswahili kusoma shahada ya Umahiri ya fani hiyo.

Katika kutekeleza makubaliano hayo awamu ya kwanza ya wanafunzi 3 wanaosoma fani ya Kiswahili wamepatiwa ufadhili wa kusoma shahada ya Umahiri ya Kiswahili katika chuo kikuu cha Dar es salaam kwa mwaka huu wa masomo.

Mkurugenzi wa Masomo ya Umahiri katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam Prof Donatha Tibuhwa amesema mashirikiano hayo yatasaidia wanafunzi kuwa mahiri katika lugha ya Kiswahili hapa nchini.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuendeleza taaluma za Kiswahili katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam Dkt Ernesta Mosha ameeleza mchakato mzima wa kuwapata washindi hao huku mmoja wa wanafunzi waliofanya vizuri katika shindano hilo wakielezea kufurahishwa kwao na udhamini huo.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad