Wanawake, Msing'ang'anie Wanaume Ambao Hawawataki

Zaidi ya watu wa 5 wameshakueleza kwamba jamaa hana time na wewe na ameshachumbia mtu mwingine hukuamini. Mungu sio Mwigulu Nchemba, siku 1 akiwa kwenye mishemishe za kuchepuka simu yake ikajipiga ukamsikia anaongea na msichana mwingine na baada ya muda ukawasikia wanapiga kwinchi kwinchi Live wakati alikuaga muda huo yuko kwenye kikao cha harusi. Mungu akaamua kukuonyesha kitu live.

Ulipomuuliza akaruka futi elfu 6 kwamba unamsingizia una kila ushahidi kwamba huyo jamaa ni kimeo ila kwa sababu akili yako ina ujibwa ulezi uliochanganywa na alizeti ukamsamehe, sasa leo amekuoa na tabia zilezile walizokuonya rafiki zako zimeendelea, unashinda unalia na kuimba Pambio la bwana tenda miujiza usiaache mpaka mwaka huu upite.

Alishatenda muujiza kukuonyesha ushahidi hukutaka kumsikia, ukapenda zaidi matarumbeta ya harusi bila kujali ndoa itakuwaje. Pole hakuna muujiza hapo, jipigie matarumbeta kwa kujitendea muujiza. Kamwe usidharau Mungu akikuonyesha (clear Signs) kwamba mtu uliyenaye ni shida. Using'ang'anie kuwa mjumbe wa bunge la katiba kama unahisi posho haitoshi achia ngazi.

Heri ukose harusi leo ujiandae kwa ndoa bora ya keshokutwa.
Tags

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Daaaa safi saaana

    ReplyDelete
  2. Daaaa safi saaana mwisho wa kupenda ni kifo

    ReplyDelete
  3. Uposahihi sana mid yalinikuta kama hayo ya kunga'ng'ania nikijua napendwa kumbe michepuko ilikuwepo imefoleni kilamoja anaambiwa ataolewa nilikua sisikii hatamtu akiniambiaje ila cku kwa macho yangu mawili tukagongana wanawake kwa skumoja ndo nilipoamua bila kuchelewa kuivua hiyo kofia bila kulazimishwa wanawake wenzangu tusiwalazimishe wanaume watupende nimaumivu makubwa sana

    ReplyDelete
  4. Daaa kweli,,,,ila si wanasema alichokiunganisha Mungu binadamu asikitenfanishe,,,lavda ndio maana wana ng'ang'ania kubaki kwenye ndoa hata kama wanasalitiwa ku keep status Muke au Mume ya Fulani.,,,,

    ReplyDelete
  5. Hilo neno mm ilinitokea na haruc kanisani na mtoto juu. Kwa Sasa Nina miaka tisa sipo naye sina muda. Nipo Muscat napiga kazi na mchumba nimepata tz. Tunapendana sana ni mcha Mungu kweli.. Yule kisokorokwinyo sijui yupo wapi nasikia ana kisulari balaa. Mungu kaniepusha na mengi. Amina..

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad