Wapiganaji wa kundi la Al-Shabaab wamevamia eneo moja la ujenzi katika kaunti ya Mandera, kaskazini mwa Kenya na kuchoma moto vifaa vinne vya ujenzi.
Polisi na mashuhuda wamesema wapiganaji hao walivamia eneo hilo mapema asubuhi ya jana na kuchoma moto vifaa vyote, lakini hakuna mtu aliyejeruhiwa katika tukio hilo baada ya walinzi wawili waliokuwa zamu kufanikiwa kukimbia.
Kamishna wa kanda ya kaskazini mashariki anayemaliza muda wake, amesema wanausalama wanafanya uchunguzi kuhusu shambulizi hilo.