Watangazaji Wanaochanganya Kiswahili na Kingereza Yamewafika


Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania  (TCRA) Kanda ya Ziwa, Francis Mihayo amesema yuko katika mchakato wa kuhakikisha anatoa elimu kwa watangazaji wa vyombo mbalimbali kanda ya ziwa ili kuwapa mafunzo maalumu yatakayowawezesha kutumia  kwa ufasaha lugha ya Kiswahili ipasavyo kwa kua watangazaji waliowengi wanasikika hewani (OnAir) wakizungumza lugha Kiswahili pamoja na Kiingereza jambo ambalo ni kinyume na maadili ya utangazaji.

Akizungumza katika maadhimisho ya miaka 25 tangu kuanzishwa kwa Klabu ya Wandishi wa habari wa Mkoa wa Mwanza, (MPC), Mihayo amesema ameamua kuandaa mafunzo  maalumu kwa watangazaji ili waweze kuzungumza kwa ufasaha lugha hiyo mama.

“Sisi kama TCRA tunasikiliza vyombo vyote Kanda ya Ziwa  kwa bahati mbaya tunasikia watangazaji wakizungumza Kiswahili na kuchanganya na Kiingereza ndiyo maana tumeamua kuandaa mafunzo haya maalumu ambayo tunaamini yatawarudisha kwenye msitari kwani sio watu wote hapa nchini ambao wanaelewa kwa ufasaha lugha ya Kiingereza,” amesema Mihayo.

Aidha, Mihayo ametoa rai kwa wamiliki wa vyombo vya habari mitandaoni kwa mikoa hiyo kuhakikisha wanajisajili.

“Kuna wandishi wa habari ambao wanamiliki vyombo  mtandaoni kama Youtube Chanel na Blogs ambazo hazijasajiliwa, nawaomba waache mara moja kwani sheria ya vyombo vya habari imeshaanza kutumika kwani kuanzia sasa tutaanza kuwakamata ili sheria ichukue mkondo wake, lazima watu watii sheria bila shuruti,” alimaliza Mihayo.

Na Johnson James -GPL -MWANZA
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kweli i akera sana. Ifanyike hivyo na kwenye uandishi pia kiswahili kimechafuka siku hizi.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad