Watangazaji Wanaochanganya Kiswahili na Kingereza Yamewafika
2
December 11, 2019
Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa, Francis Mihayo amesema yuko katika mchakato wa kuhakikisha anatoa elimu kwa watangazaji wa vyombo mbalimbali kanda ya ziwa ili kuwapa mafunzo maalumu yatakayowawezesha kutumia kwa ufasaha lugha ya Kiswahili ipasavyo kwa kua watangazaji waliowengi wanasikika hewani (OnAir) wakizungumza lugha Kiswahili pamoja na Kiingereza jambo ambalo ni kinyume na maadili ya utangazaji.
Akizungumza katika maadhimisho ya miaka 25 tangu kuanzishwa kwa Klabu ya Wandishi wa habari wa Mkoa wa Mwanza, (MPC), Mihayo amesema ameamua kuandaa mafunzo maalumu kwa watangazaji ili waweze kuzungumza kwa ufasaha lugha hiyo mama.
“Sisi kama TCRA tunasikiliza vyombo vyote Kanda ya Ziwa kwa bahati mbaya tunasikia watangazaji wakizungumza Kiswahili na kuchanganya na Kiingereza ndiyo maana tumeamua kuandaa mafunzo haya maalumu ambayo tunaamini yatawarudisha kwenye msitari kwani sio watu wote hapa nchini ambao wanaelewa kwa ufasaha lugha ya Kiingereza,” amesema Mihayo.
Aidha, Mihayo ametoa rai kwa wamiliki wa vyombo vya habari mitandaoni kwa mikoa hiyo kuhakikisha wanajisajili.
“Kuna wandishi wa habari ambao wanamiliki vyombo mtandaoni kama Youtube Chanel na Blogs ambazo hazijasajiliwa, nawaomba waache mara moja kwani sheria ya vyombo vya habari imeshaanza kutumika kwani kuanzia sasa tutaanza kuwakamata ili sheria ichukue mkondo wake, lazima watu watii sheria bila shuruti,” alimaliza Mihayo.
Na Johnson James -GPL -MWANZA
Tags
Kweli i akera sana. Ifanyike hivyo na kwenye uandishi pia kiswahili kimechafuka siku hizi.
ReplyDeleteInakera
ReplyDelete