Watoto Wawili wa Familia Moja Wafariki Baada ya Kule Kisamvu Cha Sumu

Watoto wawili wa familia moja katika Kitongoji wa Endorbo ,kijiji cha Endaghay kata ya Gidas wamefariki baada ya kula kisamvu na mihogo yenye sumu aina ya Cyanide kwa mujibu wa Daktari wa Magonjwa ya ndani kutoka hospitali ya rufaa ya mkoa wa Manyara Dr.Yesige Mutwajaa.

Akizungumzia tukio hilo mama mzazi wa watoto hao Stella Joseph aliwataja watoto hao kuwa ni pamoja na Bashiru Hamady ( 6 ) na Mwanahamis Hamady (4 ).

Alisema watoto hao walikula mihogo mibichi na baadaye walikula mihogo iliyochemshwa huku wakitumia kisamvu kama Mboga ya kula mihogo hiyo ndipo baadaye watoto walizidiwa gafla na kuanza kutapika, ndipo walipogungua kuwa kumbe walikula mihogo mibichi ikiwa na maganda yake, na hivyo kupoteza maisha siku moja isipokua walipishaba masaa mawili tu.

Kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa Manyara Paul Kasabago amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad