Waziri mkuu wa Israel adai kama si urafiki wake na Putin basi Urusi na Israel zingekuwa vitani



Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, akizungumza na redio Israel muda mchache kabla ya uchaguzi mkuu wa chama chake cha Likud amezungumzia uhusiano wake wa karibu na Putin,

“Kuna uwezekano hivi sasa tungekuwa katika vita (Urusi na Israel) kama kusingekuwepo na urafiki baina yangu na Putin. Kutokana na mazungumzo tuliyofanya miezi kazaa iliyopita tumeweza kuzuia hali hiyo”

Katika uchaguzi mkuu wa chama cha Likud, nafasi ya mwenyekiti ina wagombea 2 akiwepo Netanyahu na mbunge Gideon Saar.

Inatazamiwa kwa kiwango kikubwa  Netanyahu ataweza kutetea kiti hicho cha uongozi wa chama.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad