Wazungu Wagomea Matokeo Ya Mwakinyo, Mfilipino


LICHA ya kupanda katika viwango vya dunia, matokeo ya bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Hassan Mwakinyo na Arnel Tinampay raia wa Ufilipino yameshindwa kuwekwa kwenye mtandao wa Boxrec kutokana na kutokidhi vigezo vilivyowekwa.



Mwakinyo alimshinda Tinampay kwa pointi katika pambano la raundi kumi, uzito wa super welter ambalo halikuwa la ubingwa lililofanyika Novemba 29, mwaka huu kwenye Uwanja wa Uhuru.



Boxrec ni mtandao ambao unahusika kuhifadhi rekodi na matokeo za mabondia wote duniani ambao unamilikiwa na John Sheppard raia wa Uingereza lakini hadi kufikia jana Jumanne ulikuwa haujaonyesha matokeo ya pambano hilo.


Akizungumza na Championi Jumatano, Mwakinyo alisema kuwa kwa upande wake hadi sasa hajui kitu gani kinapelekea matokeo yake yanashindwa kuwekwa kwenye mtandao huo licha ya kupewa maneno mengi ambayo hajui mwisho wake.



“Kiukweli hadi sasa sijui nini tatizo ambalo limepekelea matokeo yangu kuchelewa kuwekwa Boxrec maana nimekuwa nikiambiwa maneno mengi kwa sababu wapo wanaosema kwamba kuna bondia wa Tanga alicheza siku ile hakuwa na kibali hivyo ni ngumu kuweka hadi kipatikane.

“Lakini niliongea na rais wa kamati ya ngumi, yeye alisema imeshindikana kupokelewa kwa kuwa hakutuma video za ushahidi Boxrec hivyo hawatoweza kuingiza matokeo hadi zipatikane kwani wao hawakuweka mtu wa kuchukua tukio hivyo lazima waende Azam kwani hata kupanda kwenye viwango kufikia nafasi ya 17 kati ya mabondia 1858 duniani imetokana na rekodi za nyuma,” alisema Mwakinyo
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad