Yaelezwa hayati Robert Mugabe aliacha mali hizi bila wosia wowote unaotaja mgawanyo, Sasa sheria kuingilia


Aliyekuwa rais wa Zimbabwe, marehemu Robert Mugabe ameacha mali mbalimbali ikiwa ni pamoja na kiasi cha pesa Dola milioni 10 (Tsh22.9bn), nyumba nne zilizopo Harare na moja kijijini kwake, magari kumi na shamba.
Mugabe hakuacha wosia wa mgawanyo wa mali zake na hivyo kupelekea hitaji la kisheria la kuchagua msimamizi wa mali hizo.



Taarifa hizo zimetolewa leo na Gazeti maarufu la The Herald la nchini Zimbabwe ambapo limeandika kwamba binti wa Rais huyo wa zamani wa Zimbabwe, Bona Chikowore alifika mahakamani mwezi Oktoba mwaka huu kuziandikisha mali za marehemu Baba yake na miongoni mwa mali hizo ni; Kiasi cha pesa ($10 million) iliyopo benki, Nyumba 4 za kuishi mjini Harare, Magari 10, Shamba 1 na nyingine nyingi.

Mwanasheria wa familia, Terrence Hussein pia amekaririwa na Gazeti hilo akiiomba mahakama kuziandikisha mali hizo, akisema yeye pamoja na familia nzima wamekosa WOSIA ulioachwa na Rais huyo wa zamani. Kwa sheria za Zimbabwe, Mali za mtu ambaye amefariki bila kuacha Wosia zitagawanywa kwa Wake zake na Watoto.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad