Yanga Waitumia Salamu SIMBA...Yaibamiza Biashara United


Klabu ya Yanga imeibuka kidedea baada ya kuitandika Biashara United bao 1-0 kwenye mchezo wa ligi kuu uliochezwa kwenye uwanja wa Taifa.

Bao pekee la ushindi kwa Yanga limefungwa na Tariq Seif dakika ya 84 akimalizia pasi ya nahodha Papy Tshishimbi akiwa ndani ya 18 na kuzamisha moja kwa moja wavuni.

 Seif ambaye aliwahi kucheza Biashara United kabla ya kusajiliwa hivi karibuni kwenye dirisha dogo ndani ya Yanga akitokea nchini Misri amesema kuwa anaona fahari kuipa pointi tatu, timu yake.

"Nimefurahi kuona nimeipa ushindi timu yangu inaamanisha kwamba ninaweza na nitaendelea kupambana kwa kushirikiana na wenzangu ili kuwa bora zaidi," amesema.

Yangaimecheza jumla ya mechi 11 inafikisha jumla ya pointi 24 sawa na Kagera Sugar inakuwa nafasi ya pili kwa tofauti ya mabao ya kufungwa ikiwa nyuma ya Simba walio kileleni wenye pointi 31 wakiwa wamecheza jumla ya mechi 12.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad