Tafsiri ya YOPE "Otimbi na Timbeli Yo: Ukiniheshimu, nitakuheshimu"

Kazi hufanyi, hutaki kutokwa jasho, umekaa kaa tu bila kujishughulisha halafu unataka watu wakupe pesa, wewe nani?

Wazazi wake hawakujui, kwao hutaki kwenda, mmekutana tu barabarani halafu unalalamika, wewe nani?

Ujinga ni wako. Upuuzi ni wako mwenyewe!

Kazi unaanza kufanya saa nne asubuhi, mchana unajidai umechoka, wakati huo wenzio wanakomaa mpaka jioni. Mshahara ukitoka unataka mlipwe sawa, wewe nani?

Mtaani hawakujui, huongei na watu vizuri halafu unataka utajwe kwenye nyimbo, wewe nani?

Ujinga ni wako. Upuuzi ni wako mwenyewe. Unajitakia mwenyewe!


Huu ni wimbo maarufu wa msanii INNOSS unaitwa Yo Pe. Uandishi wa hivi ni mzuri sana. Wimbo unaburudisha na kufundisha.

Tafsiri hiyo siyo rasmi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad