Zifahamu Pesa 8 Zenye Nguvu Afrika


Nguvu ya pesa hutambulika katika upatikanaji na uzalishaji wake, nguvu ya soko, mfumuko wa bei na soko la ubadilishwaji pesa. Dola ya Marekani huchukuliwa kuwa pesa yenye nguvu zaidi duniani hivyo hutumika kujua nguvu ya pesa nyingine

(1)Dinari ya Libya: Hii ndio pesa yenye nguvu zaidi Afrika ukiangalia thamani yake dhidi ya Dola ya Marekani na nguvu yake ya kununua (Purchasing Power) ambapo Dola 1 = 1.38 Dinari za Libya

(2) Dinari ya Tunisia: Hii ni pesa ya pili kwa Afrika ambayo Dola 1 = 3.05 Tunisian Dinari (3) Cedis ya Ghana: Ghana ni nchi pekee ya Afrika Magharibi ambayo ipo kwenye Nane Bora ya nchi nane zenye pesa yenye nguvu Afrika (Dola 1 = 5.50 Ghana Cedis)

(4) Dinari ya Morocco (Dola 1 = 9.55 Moroccan Dinari) (5) Pula ya Botswana: Pesa ya Botswana inaitwa pula na iliwekwa ili kuchukua nafasi ya Rand ya Afrika ya Kusini (Dola 1 = 10.60 Pula)

(6) Kwacha ya Zambia: Hii ni pesa ya Zambia ambayo ilichukua nafasi ya Paundi ya Zambia (Dola 1 = 11.98 Kwacha) (7) Lilangeni ya Swazi ambapo Dola 1 = 13.99 Lilangeni na (8) The South African Rands ambayo ilichukua nafasi ya South African Pound (Dola 1 = 14.18 Rands)   
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad