Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amesema kusherehekea Uhuru na wanaokandiza Uhuru ni kuhalalisha ukandamizaji.
Zitto ambaye ni Mbunge wa Kigoma Mjini aliandika ujumbe huo kupitia ukurasa wake wa Twitter kuwa kusherehekea Uhuru na wanaokandamiza Uhuru , Uhuru wa mawazo, Uhuru wa kufanya siasa na kuchagua viongozi.
“Rejea uchaguzi wa serikali za mitaa Novemba 2019, Uhuru wa habari (#Azory # Kabendera # Mwanahalisi), Uhuru wa kuishi (#BenSaanane # Lissu ni kuhalalisha ukandamizaji,” aliandika Zitto.
Kusherehea Uhuru na wanaokandamiza Uhuru – Uhuru wa Mawazo; Uhuru wa kufanya Siasa na kuchagua Viongozi ( rejea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 2019 ); Uhuru wa Habari ( #Azory #Kabendera #Mwanahalisi ); Uhuru wa kuishi ( #BenSaanane #Lissu ) ni kuhalalisha ukandamizaji.
— Zitto Kabwe Ruyagwa (@zittokabwe) December 8, 2019
Jana Chama cha Demokarasia na Maendeleo (Chadema) kimetangaza kushiriki maadhimisho ya kumbukumbu ya Uhuru wa Tanganyika ambayo kitaifa yanafanyika mkoani Mwanza.