Nyota wa mpira wa kikapaku nchini Marekani Kobe Bryant na binti yake Gianna ni miongoni mwa watu tisa waliofariki katika ajali ya helikopta iliyotokea mji wa Calabasas, California.
Bryant amefariki akiwa na miaka 41, alikuwa anasafiri na ndege binafsi aina ya helikopta ambayo ilianguka na kuwaka moto.
Mkuu wa polisi wa Los Angeles anasema kuwa hakuna yeyote aliyenusurika katika ajali hiyo.
Ripoti za awali zilisema kuwa kulikuwa na watu watano ndani ya ndege.
Bryant, ambaye ni bingwa wa Ligi ya Kikapu NBA mara tano alikuwa anatambuliwa duniani katika historia ya kuwa mmoja wa wachezaji bora zaidi wa kikapu.
Mashabiki wamekusanyika katika eneo lililotokea ajaliMashabiki wamekusanyika katika eneo lililotokea ajali
Salamu za rambirambi kutoka kwa watu maarufu na wachezaji wenzake nyota huyo zimekuwa zikimiminika kuonyesha mshtuko wa kifo cha nyota huyo wa mpira wa vikapu.
Viwanja vyote vya mpira wa vikapu nchini Marekani vilitenga muda wa kuwa kimya kwa heshima ya mchezaji huyo.
Bryant atakumbukwa katika tuzo za Grammy ambazo zilikuwa zikitolewa katika uwanja wa LA Lakers, eneo ambalo alikuwa akichezea kipindi chote.
“Tumechanganyikiwa na tuna uzuni sana kwa sasa,” alisema mtangazaji wa Grammys Alicia Keys.
“Kwa sababu mapema leo katika mji wa Los Angeles, Marekani na duniani kwa ujumla tumepoteza shujaa.
Tumesikitishwa sana kwa kumpoteza Kobe Bryant, ndio maana leo tumesimama katika nyumba aliyoijenga.”
NBA ilitoa tamko linalosema kuwa ,imesikitishwa sana na ajali iliyosababisha kifo cha Kobe Bryant na binti yake, Gianna” mwenye umri wa miaka 13.
“Kwa misimu 20 , Kobe alituonyesha kile ambacho kinawezekana kwa mtu ambaye ana kipaji na nia ya ushindi,” alisema.
Ajali ilitokeaje?Afisa wa polisi Alex Villanueva alisema kuwa helkopta inaonyesha uwa na watu tisa wakati inaanguka, na kuondoa idadi ya watu watano ambao walitajwa hapo awali na maofisa.
Katika taarifa iliyotolewa na mji wa Calabasas zilisema kuwa wamepokea taarifa hiyo kwa maskitiko makubwa sana.
“Ndege hiyo ilianguka nje kidogo ya mji wa Las Virgenes majira ya asubuhi wa saa za Marekani . Hakuna aliyenusurika, aliongeza.
Gavin Masak, alikuwa anaishi karibu na eneo tukio hilo lilipotokea, alikiambia kituo cha CBS News kuwa helkopta ilianguka.
“Haukuwa kama mlipuko lakini tulisikia kama bomu limelipuka kwa sauti kubwa. Lakini ilisikika kama sauti ya ndege au helkopta, ilisikika sauti kubwa sana, niliingaia ndani na kwenda kumtaarifu baba yangu na kumwambia kilichotokea. Hivyo nilivyotoka nikaona moshi mweusi ukitokea mlimani, ulikuwa mweusi au kama kijivu”, alisema.
Shahidi mwingine alisema kuwa alisikia injini ikiwa inashida hata kabla ndege haijafika chini.
Polisi wa LA wameonyesha picha za tukio la ajali hiyo zikionyesha gari la zima moto na moshi ukivuka kutoka milimani.
Bodi ya taifa ya usafiri imeitambua ndege iliyoanguka kuwa ni Sikorsky S-76B na imesema kuwa itatuma kikosi chake kuchunguza chanzo cha ajali hiyo.
Bryant alikuwa nani?
Bryant alicheza mpira wa kikapu kwa 20-katika viwanja vya Los Angeles Lakers. Aliacha kucheza mpira huo Aprili 2016.
Mafanikio yake ni pamoja na kuwa mchezaji bingwa wa NBA kwa mwaka 2008, mara mbili aliibuka kuwa bora zaidi ya wengine.
Vilevile alikuwa mfungaji bora wa NBA pamoja na bingwa mara mbili wa mashindano ya Olympiki.
Bryant played alikuwa akichezea Los Angeles LakersBryant played alikuwa akichezea Los Angeles Lakers
Aliwahi kupata pointi 81 dhidi ya wachezaji wa Toronto Raptors mwaka 2006, katika historia ya michezo ya NBA.
Bryant alishinda tuzo za Oscar kama mchezaji wa filamu fupi mwaka 2018 filamu hilo ilikuwa ‘Dear Basketball’, filamu ya dakika tano iliyoangazia barua moja ya
Aliwahi kupata pointi 81 dhidi ya wachezaji wa Toronto Raptors mwaka 2006, katika historia ya michezo ya NBA.
Bryant alishinda tuzo za Oscar kama mchezaji wa filamu fupi mwaka 2018 filamu hilo ilikuwa ‘Dear Basketball’, filamu ya dakika tano iliyoangazia barua moja ya michezo aliyoandika mwaka 2015.
Bryant na mke wake, Vanessa, walikuwa na watoto wengine wakike watatu ambao ni Natalia, Bianca na Capri.
Bryant alishutumiwa kwa kesi ya unyanyasaji wa kingono mwaka 2003, na binti mwenye umri wa miaka 19-aliyekuwa akifanya kazi katika mgahawa wa Coloradot. Alikanusha madai hayo, na kusema kuwa walikuwa na mahusiano ya kimapenzi ya kukubaliana.
Kesi hiyo ilifutwa baada ya mtu aliyemshtaki kukataa kutoa ushahidi mahakamani.
Ingawa baadae aliomba radhi kwa kitendo kile na kusema sababu ilikuwa msichana aliyekuwa naye hakuwa na mtazamo sawa na wake wakati walipokuwa kwenye mahusiano yao.
Watu wanasemaje kuhusu kifo cha nyota huyo?
Salamu nyingi za rambirambi zimemiminika katika mitandao ya kijamii kufatiwa taarifa ya ajali hiyo.
Shaquille O’Neal,ambaye alicheza na Bryant huko Lakers kati ya mwaka 1996 na 2004,alisema kuwa hana neno la kusema kwa sababu ya maumivu ambayo anayo.
“Ninakupenda na utakumbukwa,” aliandika katika mtandao wa Instagram wakiwa katika picha ya pamoja na jezi zao za Lakers.
Deron Williams, alikuwa mshindi wa medali ya dhahabu ya Olympiki akiwa na Bryant, aliishiwa maneno. alimuelezeaBryant kuwa mchezaji bingwa aliyewahi kucheza naye.
Ruka ujumbe wa Instagram wa dwill8
Mwisho wa ujumbe wa Instagram wa dwill8
Mchezaji wa mpira wa vikapu wa zamani Tony Parker alisema kusikitishwa kwa kifo hicho.
“Hii ni habari ya kuhuzunisha sana”, alisema rais wa Marekani Donald Trump.
Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama alimuelezea Bryant kuwa bingwa na aliyeonesha umahiri katika kipaji chake.
Usain Bolt ambaye ana medali nane za dhahabu za olimpiki alisema kuwa haamini taarifa hizi.
Mwanamuziki Kanye West aliandika katika mtandao wa twitter kuwa Bryant aliishi maisha ambayo yaliwavutia wengi.
Mariah Carey naye alisema alivyoshtushwa na taarifa hizi.
msiba wa Bryant
Baada ya kifo cha Kobe Bryant watu maarufu wameonyeshwa kuumizwa na kifo cha Kobe miongoni mwa watu hao ni pamoja na rais wa Marekani Donald Trump ambaye amesema kuwa.
“Kobe Bryant ukiachilia mbali kuwa alikuwa Mchezaji mzuri wa Basketball wa wakati wote, alikuwa ndio anaanza kuyaishi Maisha, aliipenda Familia yake sana, kifo cha Mwanae Gianna kinaumiza zaidi,Mimi na Mke wangu
tunampa pole Mkewe Vanessa na wote walioguswa na kifo hicho”