Ajikuta Matata Baada ya Kurusha Sarafu Katika Injini ya Ndege
0
January 04, 2020
Mwanaume mmoja raia wa China aliyekuwa amepanda ndege kwa mara ya kwanza, ametozwa faini kwa kurusha sarafu ya kujitakia kheri katika injini ya ndege.
Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 28 alitakiwa kulipwa dola 17,200 kama fidia ya kuingilia bajeti ya ndege hiyo inayoitwa 'Lucky Air'.
Ndege hiyo ilibidi itue baada ya kuona kuna sarafu ikiwa karibu na injini.
Lu Chao alikiri kuwa alirusha sarafu wakati akiwa anapanda ndege ya ndani ya nchi katika uwanja wa ndege wa Anqing Tianzhushan uliopo mashariki wa China, mnamo Februari 2019.
Lu alifikishwa mahakamani mwezi Julai lakini hukumu ilitangaza hivi karibuni.
Ndege ilikatisha safari yake baada ya mfanyakazi mmoja alipoona sarafu karibu na injini ya ndege.
Wakati wanaangalia hali ya usalama, waligharamika kuwahamishia ndege nyegine abiria waliokuwa wamepanda ndege hiyo.
Bwana Lu alishikiliwa katika kituo cha polisi kwa muda wa siku 10, na kushtakiwa kwa kuvuruga mpangilio uliokuwa umewekwa na hivyo alitakiwa kulipa fidia.
Mahakamani , kampuni ya ndege hiyo ya Lucky Air ilisema uwa iliwagharimu zaidi ya dola 17,600.
Bwana Lu alidai kuwa ndege hiyo ilipaswa kutoa angalizo kwa abiria kuwa hairuhusiwi kurusha sarafu katika ndege.
Hii sio mara ya kwanza kwa abiria kukamatwa kwa kurusha sarafu katika injini ya ndege.
Kumekuwa na matukio ya namna hiyo kwa miaka ya hivi karibuni.
Tags