Baada ya kusubiri kwa muda mrefu sasa hatimaye keptaini wa timu ya Taifa ya Tanzania Mbwana Sammata ametangazwa rasmi kujiunga na Klabu ya ligi kuu ya uingereza (Aston Villa) akitoa KRC Genk.
Samatta ambaye alikuwa akichezea Genk akitoa TP Manzembe jana usiku ametangazwa rasmi kuitumikia klabu ya Aston Villa hivyo kwa miaka 4 na nusu na anavunja rekodi ya kuwa mtanzania wa kwanza kucheza ligi kuu ya Uingereza.
Taarifa rasmi za usajili wa Sammata zilianza kusubiriwa kwa hamu tangu wiki iliyopita lakini kutangazwa kwake kulichelewa kutokana na taratibu mbalimbali ambazo zilikuwa bado zinafuatiliwa.
Kusajiliwa kwa Sammata Aston Villa huenda kukaiongezea mashabiki wengi timu hiyo kwan watanzania sasa wataanza kuifuatilia hata idadi ya wafuasi wao katika mitandao ya kijamii imeongezeka.
Klabu yake ya zamani ya nchini Ubeligiji imemtaki kila la kheri baada ya usajili wake kukamilika, imeposti mafanikio aliyoyapata katika kilabu hiyo na kumwambia ahsante.
Alichosema Samatta
“For me it means a lot. In Tanzania, it will be the moment they’re going to watch one of their own playing in the Premier League for Aston Villa.”