ARV’s zapunguza kasi ya saratani ya ngozi


Matumizi ya Dawa za Kufubaza Makali ya Virusi Vya UKIMWI yamechangia kushuka kwa kasi kwa Ugonjwa wa Saratani ya Ngozi ya Kaposi (Sarcoma).

Hayo yamesemwa na kaimu Mkurugenzi Idara ya Tiba katika Taasisi ya Saratani, Ocean Road (ORCI), Dkt. Mark Mseti ambaye amesema kuwa, baadhi ya wagonjwa wanaotumia dawa hizo zimewasaidia kupunguza kasi ya ugonjwa huo.

”Wadudu wa UKIMWI wanapoingia mwilini, husababisha kushuka kwa kinga ya mwili, ambapo ngozi nayo huathirika na kusababisha Saratani, lakini baada ya mgonjwa kuanza kutumia dawa imesaidia kupunguza Saratani hiyo” amesema Dk Mseti.

Kwa mujibu wa Takwimu 2018, Saratani ya Mlango wa Kizazi imeongoza kwa asilimia 32 ya wagonjwa, ikifuatiwa na Saratani ya Matiti kwa asilimia 12, na Saratani ya Ngozi ya Kaposi, Saratani ya Koo na Saratani ya Kichwa na Shingo

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad