AUNT aapa kufa na urafiki wa Wema Sepety



STAA wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel ameapa kufa na urafiki na Wema Isaac Sepetu kwani anaamini kwake ni rafiki wa kweli katika shida na raha na kama kugombana, walishagombana sana na bado wanaendelea kuwa marafiki.

Akizungumza na Risasi Jumamosi, Aunt alisema, kwa hesabu za haraka, yeye na Wema wako kwenye urafiki zaidi ya miaka kumi sasa hivyo wanajuana vizuri hata kama watakoseana, wanakaa pamoja na kuyamaliza.

“Bora nikomae na urafiki wangu na Wema, tunajua sana hata tukigombana tunajua jinsi ya kuwekana sawa na maisha yakaendelea, hivyo nahisi mpaka tunazeeka tutakuwa pamoja Mungu akitupa uhai,” alisema Aunt.

Stori: Imelda Mtema


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad