Baada ya Kuzuiwa Kuingia Ofisini kwake Hatimaye Meya wa Jiji Afunguliwa Mlango



Asubuhi ya leo Meya wa Jiji la Dar es Salaam alizuiwa kuingia katika ofisi yake na kukuta mlango wa Ofisi yake umebadilishwa Password za kuingilia hali iliyolazimu kukaa nje kwa muda.

Akizungumza na Muungwana Blog kwa njia ya simu Mwita amesema mwanzo walimfungia mlango ila kwa sasa wamemfungulia na ameingia ofisini kufanya kazi zake za kila siku kutokana na hilo ameamua kwenda mahakamani kufuta kesi aliyoifungua ya  kupinga kuondolewa madarakani  kwakua haikuwa na mashiko tena.

''Mimi bado ni meya na asubuhi ya leo nilivyofika katika ofisi yangu nikakuta mlango wa Ofisi yangu umebadilishwa Password za kuingilia nikaona hapa kutakuwa na kitu ila baada ya muda walishauriana na kunifungulia na nimeingia katika ofisi yangu na nikaamua kwenda mahakamani kwaaji ya kufuta kesi niliyoifungua awali" alisema Mwita.


Mwita alivuliwa umeya baada ya uamuzi wa kikao cha madiwani 16 wa chama tawala cha Mapinduzi, CCM, Meya Mwita alinyang'anywa gari alilokuwa akitumia na pia ofisi yake ya umeya kufungwa.

Baadhi ya hoja zilizotumiwa na madiwani wa CCM kumuondoa meya huyo wa upinzani ni pamoja na ile inayosema dereva wake alipata ajali kwa kutumia gari hiyo na pia mwenyewe alihusika na ubadhirifu wa takribani shilingi bilioni tano za umma - mambo ambayo anayakana.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad