Babu Tale Akanusha Diamond Kulipwa Mamilioni Kupanda Mlima Kilimanjaro


Meneja wa Diamond Platnumz, Babu Tale amekanusha taarifa ambazo zimeandikwa na gazeti moja nchini kwamba msanii wake alilipwa mamilioni kupanda Mlima Kilimanjaro.



Tale amekanusha uvumi huo na kudai kwamba msanii wake aligharamia vitu vingi mwenyewe kwa kuwa shughuli haikuwa na pesa kama baadhi ya watu wanavyodai.

Babu Tale amendika “Waziri maliasili na utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla @hamisi_kigwangalla mwezi wa tisa mwaka 2019 alitualika tukamuunge mkono kampeni ya #TwenzetuKileleni, ambayo ilikuwa ni kampeni ya kupanda Mlima Kilimanjaro. Hatukusita, tulikubali na kujitokeza kwa wingi sana. Waziri alituomba tumsaidie kupiga kelele mpaka tuweke alama kuwa Mlima Kilimanjaro upo nchini kwetu hapa na siyo kwa jirani ambao wamekuwa wakitangaza kuwa upo kwao. Alisema ili kampeni hii iwe na sauti kubwa zaidi tukapande sisi wenyewe. Mbali na kuutangazia umma kuwa mlima Kilimanjaro ni mali yetu, pia tutauongezea umaarufu mlima wetu ambao ni kivutio cha utalii cha kimataifa.
Wizara ilitulipia nauli ya kwenda na kurudi pamoja na chakula na tulipo fika arusha ikaja noa kuchukua wasanii basi kwa kuendelea kuisaidia serikali na kulinda heshima zetu tuliamua kujikodia wenyewe gari aina ya V8 jeusi na hakuna yeyote aliyetupa ela yani kwakifupi HATUKULIPWA wala hatukuchaji gharama zozote zile. Hata posho ya kujikimu tu hatukudai. Na wala hatukulala hoteli ya kitalii, tulilala gesti ya kawaida kabisa pale Marangu. Kwa kweli hakukuwa na anasa wala nini.
Tumesikitishwa sana kuona gazeti moja limeandika kuwa tulilipwa pesa kwa ajili hiyo. Kama kuna vita za kisiasa waendelee huko kwenye uwanja wa siasa, na siyo haki kutuhusisha sisi. Maana Mimi nilikua mmoja kati ya watu niliowashawishi wasanii na mwisho wasiku awakupata hata ela za kuachia familia zao alafu Leo mtu anatuliza akili kuandika watu wamelipwa miela tele. Msituletee siasa sisi tunamsaidia Rais kuitangaza nchi na kama mnayenu malizaneni sio mnazusha ili sisi tugombane wenyewe kwa wenyewe mtu kama @stevenyerere2 alivyo na damu mbaya ya kula pesa za watu Leo anakula mitusi kama yote sasa @hamisi_kigwangalla ukija tena uje na iyo mihela tule kweli na sio watusingizie kwa kulinda matonge yao. #TheBlackGodFather”


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad