Beki wa Yanga ajutia kadi Nyekundu aliyopata, aomba msamaha ”Sitaweza kuja kurudia tukio la aina ile”


Beki wa klabu ya Yanga, Ally Mtoni ‘Sonso’ ameomba radhi kwa kosa alilofanya hadi kupelekea kupata adhabu ya kadi nyekundu kutoka kwa mwamuzi katika mchezo wao wa hapo jana wa ligi kuu dhidi ya Azam FC ambao ulimalizika kwa mabingwa hao wa kihistoria kuambulia kichapo cha bao 1 – 0 kutoka kwa matajiri hao wa jiji la Dar es Salaam.



Ally Mtoni na Obrey Chirwa

Yanga ilishudia beki huyo akitolewa nje ya uwanja wa Taifa jijini Dar Es Salaam kwa kadi nyekundu baada ya kumkanyaga kwa makusudi mchezaji wa Azam FC katika kipindi cha pili.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mtoni ameandika, “Naomba msamaha kwa wanamichezo wote kwa kadi niliyoipata siku ya jana na tukio nililofanya kwenye mchezo wetu dhidi ya Azam FC, kweli mchezo wa mpira ni mchezo wa furaha na upendo kwa kuwa ni ajira ila changamoto za hapa na pale zipo”, amesema Mtoni.

Ally Mtoni ‘Sonso’ ameongeza “Pia naomba msamaha kwa wachezaji, viongozi wangu wa Yanga SC na pia hata wa Azam FC na hata viongozi wenye dhamana na soka letu TFF, sitaweza kuja rudia tukio la aina ile”, ameongeza.



Kikosi hiko cha Mbelgiji, Luc Eymael kipo nafasi ya nane (8) kwenye msimamo wa ligi kuu Tanzania Bara kikiwa kimejikusanyia jumla ya pointi 25, wakati vinara Simba ikiwa na alama 38 huku wapili Azam FC wakiwa na pointi 32.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad