Bilionea namba moja barani Afrika, Aliko Dangote amesema kuwa anatarajia kuinunua klabu ya Arsenal inayoshiriki Premier League ifikapo mwakani 2021.
Nigerian billionaire Aliko Dangote has again declared his intention to buy Arsenal
Dangote ambaye ndiye tajiri namba moja barani afrika kwa mujibu wa jarida la Forbes anakadiriwa kuwa na utajiri wenye thamani ya dola za Kimarekani bilioni 10.3 kupitia biashara zake.
Kwa muda mrefu bilionea huyo wa Nigeria amekuwa akihusishwa na kutaka kuichukua Arsenal ambayo inamilikiwa na Kroenke Sports & Entertainment (KSE).
Kunako mwaka 2018, Dangote aliwahi kuiambia Reuters kuwa “Tutaifuata Arsenal 2020, hatakama kuna mtu atainunua, bado tutaifuata.”
Bilionea huyo mwenye umri wa miaka 62, amekuwa akijihusisha na na miradi mbalimbali ya kibiashara ikiwemo saruji.
“Arsenal, ni timu ambayo nahitaji kuinunua siku moja, lakini ninachoweza kusema leo ni kwamba tuna dola bilioni 20 kama sehemu ya projekti na huko ndiko tunakotaka kujikita zaidi,” Dangote ameiambia David Rubenstein Show.
“Najaribu kumaliza ujenzi wa kampuni na baada ya kumaliza pengine mwaka 2021 tunaweza.” amesema Dangote.
“Siinunui Arsenal kwa muda huu. Nitainunua Arsenal wakati nitakapomaliza projekti zote kwa sababu nahitaji kuipeleka kampuni katika hatua nyingine.”