China Kujenga Hospitali Ndani ya Siku 6 Kusaidia Kutoa Huduma kwa Wagonjwa wa Corona



Mji wa Wuhan unaharakisha kujenga Hospitali mpya kusaidia kutibu Wagonjwa waliokumbwa na Virusi vya Corona ambavyo vimeshaua watu 80 na zaidi ya 870 wameambukizwa nchini humo

Kusambaa kwa virus hivyo kulianzia kwenye Mji huo ambapo sasa Madaktari wanasema Waathirika wanapanga foleni kwa muda mefu wakiwa wanasubiri huduma

Uzuiaji wa ugonjwa huo unakuwa mgumu kutokana na uchache wa vifaa vya kujilinda na baadhi ya Madaktari kuambiwa wasiende kutoa huduma wakihofiwa kupata maambukizi

Mamlaka katika Mji wa Wuhan zinasema hospitali hiyo inatarajiwa kuwa an uwezo wa kuwekwa vitanda 1000 vya wagonjwa na inatarajiwa kuanza kutumika Februari 03

Mwaka 2003, Beijing ilijenga Hospitali ya Xiaotangshan ndani ya siku 7 iliyosaidia kutibu waliougua SARS (Severe Acute Respiratory Syndrome), ugonjwa ulisababishwa na Virusi pia na kuua takriban watu 774 Duniani kwa mwaka 2002 na 2003
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad