Davido Amezijibu Tuhuma za Kupasha KIPORO na Baby Mama Wake

Davido amezijibu tuhuma za kupasha kiporo na baby mama wake, Sophia wikendi iliyopita ambapo walisafiri pamoja kwenye ndege yake kuelekea Ghana.

Davido ambaye alikuwa nchini humo kwa ajili ya tamasha la AfroNation, ameitumia insta story yake kukanusha taarifa hizo kwa kuandika kuwa alimpa lift tu mama mtoto wake kwa kuhofia kumuacha mtoto wao peke yake Lagos wakati yeye akielekea Ghana kwenye biashara zake.

"Ninataka kuacha comment fupi tu kwa blogs za kipuuzi ambazo zinadai nilimpeleka mama wa mtoto wangu kwenye mapumziko ya Sikukuu nchini Ghana. Ninaomba muache. Nyote mnafahamu kwamba nilimchumbia mchumba wangu Chioma hivi karibuni na haitakuwa na maana mimi kufanya hayo mliyosema. Mama mtoto wangu alikuwa na biashara zake Ghana akiuza bidhaa za nywele za mtoto wetu Imade." Aliandika Davido na kuendelea;

"Na mimi pia nilikuwa na show ya AfroNation. Hivyo nilimpa lift mpaka Ghana kwa lengo la yeye kutomuacha mtoto wetu Imade peke yake Lagos. Sielewi kwanini nyinyi mnasambaza taarifa hizo za uzushi, najua sitafanya chochote zaidi ni kumuumiza mchumba wangu na familia yake." Alimaliza Davido.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad